المدة الزمنية 5:32

MKUU WA WILAYA YA MONDULI MHE.ACP EDWARD JOTHAM BALELE APOKELEWA KWA KISHINDO MONDULI

بواسطة MONDULI TV ONLINE
593 مشاهدة
0
4
تم نشره في 2020/06/26

MKUU WA WILAYA YA MONDULI MHE.ACP EDWARD JOTHAM BALELE APOKELEWA KWA KISHINDO MONDULI. Leo 25/06/2020 Mkuu wa wilaya Mpya wa Monduli amepokelewa ofisini kwake na Wakuu wa Idara, Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli, Wachungaji na watu mbalimbali. Mh Dc.Acp Edward Jotham Balele amefika kutekeleza Majukumu yake ya Ukuu wa Wilaya ya Monduli kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Iddi Kimanta ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. . . . Aliekuwa Mkuu wa Wilaya Monduli ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh.Iddi Kimanta amekabidhi ofisi kwa Dc Mteule Mh. Acp.Jotham Balele ambaye ni Mkuu mpya wa wilaya ya Monduli. Mhe. DC Balele ameahidi kumpa ushirikiano Mkuu wa mkoa Arusha na pia Kuwapa ushirikiano watumishi wa idara zote. . . . Mkuu wa wilaya amenza kazi Mara Moja kwa Kuendelea kusikiliza Wananchi na kutatua changamoto zao wanaofika ofisini kwake. Pia amefanya ziara ndogo kwa kutembea Kituo cha Polisi Monduli na kuzungumza na maafisa wa polisi. . . . Dc Balele amdhamini Mgombea Uraisi Mheshimiwa Raisi John Pombe Joseph Magufuli mara baada kufika Ofisi za Chama Wilaya ya Monduli kwa mara kwanza. MONDULI MPYA DC BALELE KARIBU MONDULI. Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Monduli. 25/06/2020. Elifuraha Raphal(Kaburu).

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 2